www.shijamovies.blogspot.com

www.shijamovies.blogspot.com

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460
Get Swimming Training from Experts www.marineswimmingclub.blogspot.com

November 30, 2013

BONANZA KATI YA BONGO MOVIE NA BONGO FLEVA

 Ni wakati wenu mashabiki wa bongo movie na bongo fleva.Jumapili kutakuwa na mechi  ya mpira wa miguu kati ya bongo movie na bongo fleva.


 bonanza hilo litakuwa siku ya jumapili katika uwanja wa TCC Chang`ombe kuanzia asubuhi.Fika ujionee viwango vya wasanii wetu katika mchezo.


Bongo movie wamepania kushinda mechi hiyo ili kulinda heshima, kwani mara ya mwisho katika tamasha la matumaini ililofanyika mwezi wa 7 mwaka huu bongo fleva iliwachapa bongo movie 2-1.



November 29, 2013

STIKA ZA TRA.


Wasanii wa bongo movie kwa umoja wao wametoa malalamiko yao kwa mamlaka ya mapato nchini TRA kwa kuchelewesha kutoa  stika za ushuru kwa haraka.



 Wasanii haowakiongozwa  na mwenyekiti wao Vicent Kigosi “Ray” wamesema kitendo cha TRA kuchelewesha kwa upatikanaji  wa stika hizo kwa wakati unasababisha kuchelewa kuingia kwa kazi mpya sokoni.


Tangu  kulasimiswa kwa secta ya filamu na serikali kuanzia novemba mosi mamlaka ya mapatoTRA wameingia stika chache nchini na kusababisha mlundiko wa kazi nyingi kushidwa kuingia sokoni kwa wakati.

November 28, 2013

Snura kuachia kibao kipya.

Msanii wa filamu na mwimbaji wa muziki wa mduara Snura Mushi anakaribia kutoa kibao chake kipya hivi karibuni.


Snura ambaye anatamba na nyimbo zake mbili ambazo ni “majanga” na “nimevurugwa”,Amekataa kutaja jina la kibao chake kipya.


 Amesema mashabiki wake wakae mkao wa kula.


Linex na MH. Zitto Kabwe.


Wakati kamati ya chadema ilipo kaa kutoa taarifa  ya  kuwavua  vyeo   walivyokuwa  navyo Zitto Kabwe  na DR Kitila Mkumbo.


 Mmoja wa wasanii wa muziki wa bongo fleva  Sande Mangu kwa jina maarufu kama “Linex” amemtaka mbuge huyo  kuyapokea hayo kama changamoto  katika nafasi yake ya kisiasa.


November 27, 2013

Aunt Ezekieli mahakamani.

Mwigizaji chipukizi Yvone Bigilwa jana alipanda tena mahakamani katika kesi ya kumpiga na kumjeruhi mwigizaji mwenzie Aunt Ezekieli.




  Wakati wa kusomwa kwa kesi  hiyo Aunt Ezekieli hakuwepo mahakamani hapo.

Mrisho Mpoto ajiandaa kutoa filamu.


Mwimbaji  Nguli wa mashairi hapa nchini Mrisho Mpoto  anatarajia kufanya  filamu yenye vionjo vya asili.


 Mpoto amesema ndani ya filamu hiyo kutakuwa na ngoma za asili na nyimbo za asili.

 Hivi karibuni  msanii huyu na wenziwe wanatarajia kuingia kambi kwa ajili ya kufanya mazoeziya filamu hiyo.


November 22, 2013

Thea atoa la rohoni



Mcheza filamu za bongo Ndumbangwe Misayo “Thea”amefunguka na kusema kuwa Maisha ya ndoa ni Maisha magumu sana kama ndani  ya nyumba wana ndoa hawasikilizani na kuelewana. 

Thea na mume wake mike siku za hivi karibuni  ilitokea tetesi kuwa ndoa yao imevunjika. Thea ambaye kwa  hivi  sasa amerudi kwa wazazi wake kwa mapumziko anasema kuwa kama angekuwa anajuwa asingetaka kuolewa. 

Thea anasema kuwa  kinachofanya ndoa yao isivunjike ni yesu kristo anawasimamia.



Mzee Yusuf ampongeza Shija.



Mwimbaji wa muziki wa taarabu Mzee Yusuf amemsifia msanii wa bongo movie Deogratius  Shija kuwa ni msanii anayeweza kubadilika kiuchezaji.




Mzee Yusuf  ameendalea kufunguka  kuwa  tangu aanze  kuzifuatilia sinema za Shija ni msanii pekee anayebadilika na kucheza  nafasi yoyote ile tofauti  na wasanii wengine wanaopenda kucheza  nafasi za ubosi na utajiri tu.

Mzee yusuf ameshauri wasanii wa filamu wabadilike  ili waweze kufika mbali zaidi.


Van vicker awapa pongezi bongo movie.



Mwigizaji   nguli kutoka Ghana Van Vicker amewapa pongezi wasanii wa filamu  hapa  nchini  kuwa wanauwezo mkubwa wa kuigiza.



Van Vicker akiwa location


Msanii huyo  ambae alikuwepo hapa nchini kwa ajili ya kucheza filamu ambayo  imeandaliwa  na kampuni mpya ya usambazaji ya proin promotion. 


Mbali na pongezi hizo pia amewashauri  wasanii wa bongo kuandaa filamu kwa lugha ya kingereza kitupu ili awatafutie  soko nchini Nigeria na Ghana.



Rufaa ya akina Babu sea yagonga mwamba tena.



Wanamuziki  wa dansi  nchini Tanzania  ambao ni baba na mwana“Babu Sea” (Vick Nguza) na Papii Kocha sasa  wanasubiri  huruma  ya  Rais  wa  jamhuri  ya  muungano  wa Tanzania, kutokana na mahakama ya rufaa  kupitia  rufaa  yao na kuitupilia mbali kwa madai kwamba haikuwa na jambo jipya tofauti na rufaa ya awali.

Hivyo wataendelea kutumikia kifungo cha Maisha jela kwa mujibu wa katiba ya Tanzania.Mkuu wa nchi anayomamlaka ya kutoa msamaha  kwa wafungwa.
 Kilicho baki sasa watanzania wanasubiri huruma hiyo kuwawezesha kurudi uraiani.



November 20, 2013

Jacob Stephen (JB) na sintofahamu!


Muigizaji Mkongwe  na  kipenzi   cha  watu  na  ambaye ni  balozi wa Kampuni Ya Simu  Ya  Airtel Jacob Stephen  kwa  jina  maarufu   kama JB   amejikuta katika  hali  ya sinto  fahamu   baada  ya mabango  makubwa   yaliyokuwa  na  picha  yake  yakitangaza  kampuni   hiyo  yakishushwa  bila maelezo Yoyote.




Hivi  karibuni  kupitia  kipindi cha Gossip  cha Sudi Broun  kinachoruswa  na  kituo  cha Redio  cha Clouds  inasemakana  msanii  huyo  alikamatwa  ugoni   Mkoani Dodoma.




Wema Sepetu ajisalimisha Mahakamani.


 Ni baada ya mahakama kutoa hati ya kumkamata muigizaji Wema Isack Sepetu kutoka na madai ya kutohudhulia mahakamani mara mbili  katika kesi inayomkabili ya kumtukana na kumjeruhi meneja wa hoteli ya Mediterania Bwana Goodluck Kayumbu.




Wema katika utetezi wake aliikabidhi mahakama cheti cha kifo cha baba yake mzee Isack Sepetu na kuiambia mahakama alishidwa kuhudhuria mahakamani kwasababu alikuwa anauguliwa na baba yake ambae kwa sasa ametangulia mbele za haki.



katika utetezi wa pili”wema alisema siku ya tukio alikuwa amelewa sana na alichokifanya ilikuwa ni pombe baada ya kugundua amefanya kosa hilo alifanya jitihada za kumuomba msamaha Bwana Goodluck Kayumbu lakini meneja huyo alikataa na kulifikisha jambo hilo mahakamani”



Wiki ya majonzi kwa tasnia ya filamu nchini Tanzania!



 Ni mwaka mmoja tangu JOHN STEPHANO MAGANGA & HUSSEIN RAMADHAN walipotangulia mbele za haki


JOHN STEPHANO MAGANGA 


kwa wapenzi  na wadau wa tasnia ya filamu hapa nyumbani Tanzania itakuwa ni wiki ngumu kwao tangu kuondokewa kwa waigizaji wa filamu hapa tanzania. wiki hii ndiyo wiki ya wasanii JOHN STEPHANO MAGANGA na HUSSEIN RAMADHAN kama sharo milionea walipotangulia mbele za haki tarehe  24/11/2012 marehemu John Maganga alifariki dunia katika hospitali ya taifa muhimbili baada ya kuuguwa kwa siku mbili na kufariki kwa muujubu wa taarifa za madaktari  wa hospitali ya taifa muhimbili    John Maganga alifariki kwa ugonjwa  wa kongosho.



HUSSEIN RAMADHAN



Siku mbili baadae 26/11/2012 tasinia ya filamu ilipoteza msanii mwingine HUSSEIN RAMADHANI kwa jina maarufu kama Sharo Milionea alifariki kwa ajali ya gari alipokuwa ansafiri kuelekea kijijini kwao Muheza  Mkoani Tanga.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi AMIN!

November 19, 2013

Muigizaji wa Bongo Muvi Niva akumbwa na dhuruba!


 Niva akumbwa na dhoruba!


Muigizaji wa filamu za bongo  hapa nchini Zuberi Mohamed (NIVA) amejikuta katika hali ngumu baada ya kuibiwa vifaa vyote vya ndani ya gari Kama radio, power window, na vingine vingi  kwenye  gari yake aina ya  Toyota Alteza.





Inasemekana kuwa  wizi huo ulifanywa na  vibaka usiku gari hilo lilikokuwa limeegeshwa.

Kwa maelezo yake vibaka hao   walifanya wizi huo usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.





Niva ambae kwa sasa anafahamika sana kwa filamu ya “GUBU LA MUME” ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo hicho na kuwa amesharipoti polisi.



November 16, 2013

Mike Sangu apata pigo kubwa!


                             Mike Sangu ampoteza Dada yake mkubwa!


Muigizaji  wa  filamu za bongo Mike Sangu amepata pigo la kuondokewa  na dada yake mkubwa aitwae Salma Sangu

             Mama wa marehemu pichani chini 


 Mike akipembelezwa na mke wake Thea (pichani chini)


Mike Sangu akisaidiwa kwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa dada yake




         Baadhi ya waombolezaji  wakiwa katika  mazishi  wa dada yake Mike Sangu


Chini muombolezaji akiweka udongo kwenye kaburi

 Dada yake alifariki  usiku wa kuamkia Jumatano katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.


Tunampa pole sana Mike Sangu kwa msiba huu!

November 15, 2013

Ney Wamitego kutoa kitu kipya "NAKULA UJANA"

 Ney Wamitego kutoa kitu kipya "NAKULA UJANA"


 Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki  Maarufu kama Ney wa Mitego anatarajia kusambaza kazi yake mpya inayojulikana kwa jina la "NAKULA UJANA" Ney ambae anatamba na wimbo wake wa "Salaam zao".





Ney amejisifu kuwa yeye ni mtu makini katika utunzi wa nyimbo zake na wala habahatishi.