www.shijamovies.blogspot.com

www.shijamovies.blogspot.com

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460
Get Swimming Training from Experts www.marineswimmingclub.blogspot.com

December 31, 2013

MKUTANO WA KURASIMISHA SEKTA YA FILAMU NA MUZIKI

Mkutano wa kurasimisha sekta ya filamu na muziki uliofanyika Jana katika ukumbi wa vijana kinondoni jijini Dar umeondoka na Azimio moja kuu tarehe 23 January 2014 wasanii wa filamu na muziki watafanya maandamano kuanzia vijana mpaka wizara ya habari utamaduni na michezo kwenda kukabidhi Sera ya filamu na muziki ili iperekwe bungeni kutungwa sheria.mkutano huo uliandaliwa na TRA. COSOTA. BASATA.TAFF na Shirikisho la Muziki.

WASTARA AMLIZA MAMA SAJUKI

Mwigizaji wa bongo movie na Mke wa marehemu Sajuki amemfanya Mama Mzazi wa marehemu Sajuki kutokwa na machozi baada ya kumuona Wastara. Wastara yupo songea mkoani ruvuma kwa ajili ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Mume wake Sajuki itakayofanyika Alhamisi wiki hii.

December 27, 2013

BONGO MOVIE KUFANYA MAANDAMANO

Wakati wasanii wa filamu wakiwa wamepanga kufanya maandamano ya kupinga wizi wa kazi za wasanii kesho jumamosi katibu mkuu wizara ya habari utamaduni na michezo amewaomba wasanii hao kusitisha maandamano na kuwaita wizarani kwa majadiliano na kuangalia namna ya kulitatua tatizo hilo.




Akizungumza katika blog hii msanii wa filamu hapa nchini Issa Musa " cloud" amethibitisha kupokea barua hiyo ya mwaliko siku ya jumatatu 30/12/2013

WASTARA AMKUMBUKA SAJUKI

Zikiwa zimebaki Siku 6 kutimiza mwaka mmoja tangu marehemu sajuki atangulie mbele za haki.


Msanii wa filamu na aliyekuwa mke wa sajuki Wastara yuko njiani kuelekea songea kijijini kwa marehemu sajuki kwa maandalizi ya dua ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu sajuki alipofariki.

Marehemu sajuki alifariki tare he 2/1/2013 katika hospitali ya muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.Wastara anaomba mashabiki wake wamuunge mkono katika dua hiyo


December 23, 2013

ZAWADI YA X-MASS KUTOKA KWA MALIKIZOH

 Msanii  wa kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizoh ameachia ngoma yake mpya ijulikanayo kama SUPER HERO.

“Napenda  kuwaomba  mashabiki  wangu wa  muziki  kuendelea kuniunga mkono katika kazi zangu nyingine zijazo”alisema malikizoh. 




FUNGUA HAPA UONE HIYO KITU KALI>>>>

https://www.youtube.com/watch?v=hO0d3pGmCVY&feature=youtube_gdata_player


JACKLINE WOLPER ARUDIA DINI YAKE

 Msanii wa filamu za kibongo mwanadada Jackline Wolper amerudi katika dini yake ya zamani ya kikristo.
Mwaka uliopita ilisemekana kuwa mwana dada huyo alibadilisha dini kutoka na mpenzi wake wa zamani Bwana Abdala Mtoro"Dallas" kuwa ni Muislamu.


Kwa sasa mwana dada huyo kila jumapili anashika biblia na kuingia kanisani.



December 21, 2013

HEMED NA MLELA HAWANA UGOMVI

 Kutokana na tetezi zilizozagaa mjini hapa kuwa waigiza wa filamu za kibongo Hemed Suliman”PHD” na Yusuf Mlela kuwa wana bifu la kufa mtu si za kweli kuthibitisha hilo wasanii hao.
Walikutana katika ofisi za Steps Entertaiment kampuni inayosambaza filamu za kibongo na kupeana mikono kwa furaha tele.

BONGO MOVIE KUFANYA MAANDAMANO


Wakati wasanii wa filamu nchini wakifikiria kurudi kwenye michezo ya tamthilia wameamua kufanya maandamano katika mkoa wa dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 28 mwezi huu.

 Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake Issa Musa maarufu kama “cloud” amesema lengo la maandamano hayo ni kupiga kelele juu ya wizi wa kazi za wasanii ili serikali isikie kilio chao na kutoa sheria kali kwa wale wote watakaobainika kuiba kazi zao wakati huo huo jeshi la polisi kanda ya DSM tayari imeisha toa kibali cha maandano hayo.

December 19, 2013

JELA IMENIFUNZA MENGI.

Mwigizaji Mrembo wa Bongo Movie Elizabeth Michael “lulu” amesema kitendo cha kukaa mahabusu takribani miezi kumi amejifunza mambo mengi sana.


 Lulu ambaye alikuwa mahabusu ya segerea baada ya kifo cha marehemu Steven Kanumba kwa sasa lulu anatamba na filamu yake ya Foolish Age.


December 18, 2013

WASANII KURUDI KWENYE TAMTHILIA

Baada ya wizi wa kazi za wasanii kupamba moto nchini,makampuni ya usambazaji  wa Filamu kutishia kufunga makampuni yao. 
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wanataka kurudisha  michezo  ya TV Kama zamani.kipindi cha nyuma kulikuwa na makundi kama Kaole ,Mambo hayoFukuto yaliyofanya  vizuri sana kwenye luninga. Msanii maarufu nchini DR Cheni alisema ni bora wasanii tukarudia michezo ya TV kuliko filamu ambazo zinaibiwa na kupata hasara.


 Moja kati ya michezo  ya kipindi kile iliyokuwa inachezwa na Kaole  Sanaa Group  ni mchezo wa KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA.Katika kuongezea mkazo juu ya hilo msanii nguli Single Mtambalike "Richie Richie"  amesema wasanii tutumie fursa ya hizi TV zinazoendelea kuanzishwa kupeleka kazi ambazo hazitatuumiza kichwa kwa wizi huo. 


Katika kufanya kwa vitendo msanii mnene hapa nchini JB amesema yeye anaingia kambini kutengeneza tamthilia.

 


December 17, 2013

TUNDA MAN AJA NA ZAWADI YA MWAKA MPYA

 Msanii wa bongo fleva Khalid Ramadhani ametoa nyimbo yake mpya inayojulikana kama msambingungwa. 


Tunda amesema jina la msambingungwa ni jina la msichana aliyekuwa anamsumbua kwa muda mrefu




WEMA MAHAKAMANI TENA

Baada ya Mahakama ya Mwanzo kawe kumuachia kwa faini ya laki moja mwana Dada Wema Sepetu mlalamikaji katika kesi hiyo bwana Gudluck Kayumbu ameibuka na kusema hakuridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo na anakusudia kukata rufaa. 



Wapenzi wa Mwana Dada Wema Isaack Sepetu wameibuka na kusema Meneja huyo anatafuta kick kupitia jina la Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu





December 16, 2013

Matukio ya mwaka 2013 => Bongo movie wampoteza sajuki

2 /01/ 2013 tulimpoteza msanii nguli wa Filamu nchini Juma Kilowoko Sajuki.




Bado siku chache kutimiza Mwaka mmoja tangu tasnia ya Filamu kuondokewe na msanii maarufu Sajuki.



DEAGRATIUS SHIJA ateuliwa kuwa meneja wa MALIKIZO

 Msanii  wa kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizo amemteuwa Muigizaji wa bongo movie Deogratius Shija kuwa msimamizi wa kazi zake za muziki.


Deogratius Shija ndio meneja wa Malikizo



December 13, 2013

MIKE SANGU APATA USUMBUFU.


Aliyekuwa Mume wa muigizaji wa Bongo Movie Ndumbangwe Misayo “Thea” Mike Sangu amefunguka na kusema kuwa tangu waachane na mkewe Thea amekuwa akisumbuliwa na kupigiwa simu na wanawake wanaomtaka kimapenzi.

“Tangu watu walipojua tumeachana na Thea siku za hivi karibuni nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanawake wengi”

Alipoulizwa kama anampango wowote wa kurudiana na Thea Mike alijibu "namuachia mungu tu kwani sikuona sababu yoyote ya Thea kuondoka nyumbani kwangu. kwakweli napata shida sana nimekuwa mtu wa kula hotelini na sina muda mzuri wa kula nyumbani kwangu ili linanipa shida sana " ndoa ya Mike  na Thea ni ndoa iliyodumu miaka mitatu tu alisema Mike



December 12, 2013

MALIKIZO KUTOA SUPER HERO


Msanii  wa kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizo anatarajia kuachia ngoma yake mpya itakayojulikana kwa jina la SUPER HERO.Malikizo anaendelea kusema ngoma yake hiyo ni moja kati ya ngoma kali aliyoifanyia katika jiji la Perth nchini humo.



Malikizo anaendelea kufunguka na kusema kuwa SUPER HERO NI ZAWADI ya X-MASS kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva. ”Ngoma ya SUPER HERO itakuwa hewani katika vituo mbalimbali vya Redio na TV.  Malikizo yupo nchini Australia kwa masomo ya Muziki na Filamu.



“Napenda kuwaomba mashabiki wa muziki kuipokea ngoma yangu hii mpya’ Alisema Malikizo.

BURIANI MZEE HILUKA.

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na rais  wao wa TAFF Bwana Saimon Mwakifamba jana ni miongoni mwa watu waliojitokeza kumzika Baba mzazi wa katibu wa shirikisho la Filamu Tanzania “TAFF” bwana Bishop Hiluka uko boko jijini Dar es salaam.

Mzee Hiluka alifariki katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa ugonjwa wa moyo.


“Kwakweli nimefarijika sana kuwaona wasanii wenzangu wamekuja kumzika Baba yangu” alisema Bishop huku akitoa machozi kwa uchungu





December 11, 2013

TAARIFA ZILIZO ENEA KUWA MZEE SMALL KAFA SI ZA KWELI NI UONGO..HII NDO KAULI YA MTOTO WAKE MUDA HUU

KUNA TAARIFA ZIMEENEA USIKU HUU KUWA MZEE SMALL KAFARIKI,HIZO TAARIFA SI ZA KWELI BALI NI UONGO MTUPU ULIO SAMBAZWA MITANDAONI..MTANDAO HUU 
WA THECHOICE ULIWEZA KUONGEA NA MTOTO WAKE USIKU HUU AITWAE MAHAMOUD NA KUTHIBITISHA KUWA BABA YAKE YU HAI HAJAFARIKI.  "BABA YU MZIMA NA WALA HAJAFARIKI KWANI NIMETOKA KUMJULIA KHALI MDA SI MREFU NA NI MZIMA ANAENDELEA VIZURI NA HIZO TAARIFA NI ZA UONGO "

http://www.thechoicetz.com/2013/12/breaking-newzzztaarifa-zilizo-enea-kuwa.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29&m=1

December 9, 2013

KATIBU WA TAFF APATA PIGO

Katibu wa shirikisho la  filam Tanzania “TAFF”Bwana Bishop Hiluka amepata  pigo baada ya kufiwa na baba yake mzazi Mzee Hiluka.




WASTARA AFUNGUKA

Wakati wadau wa tasnia ya filamu nchini wakimshauri msanii wa filamu Deogratius Shija kumuoa msanii mwenzie  Wastara Juma. 



Kuna tetesi kuwa  mwana dada huyo  mjane amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha ACTION  and CUT bwana Bond bin sinnan. Wastara amesema kuwa  muda siyo mrefu mrefu atamtambulisha mpenzi wake mpya.




December 6, 2013

WIZI WA KAZI ZA WASANII.

kutokana na wimbi kubwa la kazi za wasanii hususani filamu imesababisha baadhi ya makampun ya wasambazaji kufunga virago.akizungumza kwa niaba ya wenzao mtayarishaji na msanii wa filamu za kibingo Vicent Kigosi “RAY” amesema hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la wizi wa kazi za filamu.


Ray ameendelea kusema kuwa kama hali hii itaendelea hivi wasambazaji wote watayafung makampuni zao na hakutakuwa na filamu hata moja sokoni.Ray anaomba wadau pamoja na serikali kupiga marufuku kwawizi wa kazi za wasanii kame wanavyopiga vita uuzaji wa madawa ya kulevya       



MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

Katika kukabiliana na janga la ukimwi nchini taasisi ya MKAPA FOUNDATION imewataka wasanii wa filamu na wanamuziki  wa  kizazi  kipya  kushikamana kwa pamoja na kuelimisha jamii katika suala zima la maambukizi ya virusi vya ukimwi.

 Akifungua majadiliano hayo kati ya waandaaji wa MKAPA FOUNDATION  na wasanii hao naibu waziri wa wanawake  jinsia na  watoto MH UMMY MWALIMU ameomba  wasanii kufanya tungo za kuelimisha jamii kuhusu kujikinga na maambukizi ya ukimwi kwani ukimwi upo.


 Akiendelea kufafanua zaidi MH WAZIRI  amesema wasanii wana nguvu  ya ushawishi mkubwa katika jamii ya leo.




 MKAPA FOUNDATION iliandaa majadiliano hayo  katika siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika katika hoteli ya protea ya jijini Dar es salaam.





R.I.P NELSON MANDELA 1918/2013

Wasanii wa bongo fleva na bongo movie wanatoa pole kwa familia na serikali ya Africa kusini kwa kuondokewa na mzee wao Nelson Mandela.





MUNGU AILAZE ROHO YA NELSON MANDELA MAHALI PEMA POPONI AMINA