www.shijamovies.blogspot.com

www.shijamovies.blogspot.com

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460
Get Swimming Training from Experts www.marineswimmingclub.blogspot.com

Darasa La Sanaa

DARASA LA SANAA SEHEMU YA TATU


Ndugu zangu naamini wote ni wazima wa afya njema.

Suala ninalozungumzia leo litawahusu sana wasanii wa tasnia hii ya picha jengefu. Kama nilivyoeleza siku zilizopita kuwa sana hii ni kazi kama zilizo kazi nyngine kala kazi ina miiko na sheria zake za kazi.

Kama ilivyokuwa katika kazi zingine kuwa huwezi ukaenda hazini kwa muda wako unaotaka wewe au huwezi kwenda kazini ukiwahi umelewa au  ukwenda kazini alafu ukiagiza pombe na kuanza kunywa muda kazi  lakini tabia hii inajitokeza kwa baadhi yawasanii wetu wa hapa nyumbani Tanzania.

Sasa sijui wanafanya hivi kwa sabababu  hawajijui wao ni kina nani? Au wanafanya makusudi kwasababu hawajui kama hiyo ni kazi kama kazi nyingine.

Kwanini wasitenge muda wa kazi na muda wa kufanya hiyo mambo yao. Hivi karibuni nimeshuhudia msanii mkubwa kwa umri na msanii mkubwa  kwenye  tansia hii ya filamu akifikia location uishia bar na kuagiza pombe na kuanza kunywa hii ndiyo ikanifanya nichukue kalum na kuandika haya yote.


Napenda kwasababu wasanii wote  popote pale walipo nchini kujiheshimu na kuheshimiwa hii ni kazi, ili tujenge heshima mbele ya jamii yetu inayotuzunguaka.


DARASA LA SANAA SEHEMU YA PILI

Kazi ya sanaa ni kazi ya taaluma kama zilivyo kazi zingine lakini kutokana na mfumo wa elimu wa tanzania somo la films halijawekwa ktk mitaala ya kielimu hapa tanzania na bahati mbaya vyuo vinavyotoa elimu ya juu ya filamu ni south africa na ghana pekee


DARASA LA SANAA SEHEMU YA KWANZA

Ndugu zangu kwanza ningependa  kuwasalimu na nina amini kuwa wote ni wazima.

Napenda kwa leo nizungumzie swala dogo sana katika sanaa hasa hii yangu ya filamu. Leo  napenda kutaka kutafsiri neon  mwigizaji  nimekuwa nikipita sehemu nyingi  ndani ya nchi  hii ninaitwa muigizaji au huyu anaigiza.  

Tafasiri ya neno ili muigizaji inanitia shaka kidogo  mfano waingereza wenzetu wanatumia neon  actor  au actress. neno actor ni kwa muigizaji mwanaume  na neon  actress ni kwa muigizaji mwanamke  lakini hapa nyumbani  wote tunaitwa waigizaji.  Tafsiri ya neno actor au actress ukiileta katika lugha  yetu ya kiswahili  unaweza kupata tafsiri zisizo rasmi nyingi sana napenda kutoa  mfano mmoja   mdogo sana: 

Mfano ukisimama mbele ya kioo nafikiri utakacho kiona ni taswira halisi ya muonekano wako mwenyewe, utakacho kifanya chochote ndivyo hivyo hivyo ile  taswari itakavyo fanya, je kioo nacho kitakuwa kinaigiza? Au kioo kinafanya  kile ambacho wewe unakifanya  kwa  wakati  ule?
Hapa ndipo napata shida ya neno muigizaji!

huyu muigizaji anaigiza nini? au anafanya mambo ambayo yanatokea katika  jamii inayomzunguka?sasa kwanini umwite mwigizaji?

Wakati mwingine napenda kukubaliana na waingereza kuita waingizaji actor / actress.
Kwa leo nitaishia hapa tutakutana tena wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment