Featured Posts

www.shijamovies.blogspot.com

www.shijamovies.blogspot.com

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460

Marine Tanzania Swimming Club Call: +255 655 461 460
Get Swimming Training from Experts www.marineswimmingclub.blogspot.com

May 12, 2014

B12 ACHAFUA HALI YA HEWA

B12 ACHAFUA HALI YA HEWA BAADA YA KUMWAMBIA OMMY DIMPOZI KUHUSU VIATU VYAKE KAMA NI VYA KIKE AU VYA KIUME?

                               


Kwenye mtandao wa twitter, mtangazaji wa Clouds FM Hamisi Mandi au wengi tukimfahamu kama B12 "B-Dozen" amemuuliza swali la kizushi Ommy dimpoz kuhusu viatu vyake alivyo vaa..
nahiki ndicho alichoandika... B12 nakuweka picha ya viatu hivyo..
"Hivi ndo Viatu Vya dimpoz, si kwa ubaya tunaomba ufafanuzi ni Vya kike au kiume?"
We unaonaje Msomaji?





SHAA AFUNGUKA KUHUSU NGOMA YAKE YA “SUGUA GAGA”

  
Shaa, mkali wa "sugua gaga” afunguka kuhusu siri ya uzuri wake na mambo mengine kibao.... "i have many pair of shoes and sometime huwa navigawa kwa ndugu zangu"


4. Muonekano gani wa mavazi unautamani kuujaribu?
Natamani sana kujaribu muuonekano wa gosick fashion mara nyingi wanavaa sana Rock stars wa Marekani utamkuta kavaa full black from top to bottom.
5. Celeb gani wa ki-Bongo wanakuvutia kwa mavazi yao?
Actually Madam Rita na Nancy Sumari all the time navutiwa sana ninapowaona kutokana na uvaaji wao.


6. Una pair ngapi za viatu?
I have many pair of shoes, am so crazy man and sometime huwa navigawa kwa ndugu zangu coz siwezi kukaa na kitu bila kukivaa.


7. Uzuri wako unatokana na nini?
Ni kujiweka naturally bila kujirundika make up, so napenda sana kuwa simple coz is the best to me.



May 10, 2014

WEMA SEPETU APEWA ONYO KALI NA STEVE NYERERE

MWENYEKITI wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Stive Nyerere’ ameibuka na kumuonya Wema Sepetu kupiga kazi na kuepuka umaarufu bila kazi.


 

 Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Stive Nyerere’.

Nyerere amemtaka Wema aachane na skendo za kila kukicha kwani hazina maana kama kazi ya sanaa aliyoichagua kama njia ya kumuingizia kipato.




                  Wema Sepetu akiwa na Diamond Platinum.
“Kwanza nampongeza sana Diamond kwa tuzo zote alizopata kwa kuwa alistahili lakini Wema naye anapaswa kuiga mfano, vinginevyo atakuwa maarufu bila ya heshima,” alisema Steve Nyerere.











ENDLESS FAME FILMS WATOA KAULI KUHUSIANA NA UGOMVI WA WEMA NA KAJALA

Kampuni ya filamu ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, leo imetoa kauli yake kuhusiana na ugomvi wa mmiliki wa kampuni hiyo na aliyekuwa rafiki yake wa karibu Kajala Masanja.

Maneja wa kampuni hiyo, Martin Kadinda ametoa msimamo huo kupitia mtandao wa Instagram.


“Good morning all of you…. I just woke up Like “Hasiraless” kwakuwa hili vugu vugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema sepetu (myclient) na Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu endless fame.

Katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndo lililotokea baina ya hawa wawili. Lakini katika kipindi hicho cha so called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu, kuna media coverage juu ya hawa wawili na wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi… ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na kajala sema tu Kwa sasa anahitaji space…… tukawa tumefunga mjadala huo.


Endless fame(wema sepetu) haijawahi kutamka lolote swala la mahusiano ya kajala na mtu yoyote, EndlessFame haijawahi kudoubt urafiki wa kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya wema au wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki… hapana hapana… Hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona.

Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wanaushahidi kutoka endless fame au Kwa mtu wa karibu na wema. Team wema wote waliopo insta sijawahi kuona hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza and hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati Kwa wema.

Poleni Kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya instagram tuwaache huku huku ukiyasikiliza utashindwa kumwamini mama yako mzazi.”

Hivi karibuni Kajala alisema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.


Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii, Kajala alisema amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. Alidai kuwa pamoja na ugomvi wao kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.

Kuhusiana na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi hana chochote. “Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” alisema.

Kajala alikiri kuwa kukosana kwake na Wema kumeathiri maisha yake. “Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nammiss,” alisema na kueleza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo alisema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe, ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena.

DIDA AZUA TIMBWILI BAADA YA KUNG'ANG'ANIWA NA MWANAMKE MWENZAKE

DUNIA ina mambo! Prizenta wa Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ amezua timbwili baada ya kung’ang’aniwa na mwanamke mwenzake aliyedaiwa kutaka kumshawishi afanye naye mapenzi ya jinsi moja (usagaji).
Dida alikumbwa na ishu hiyo, Alhamisi ya wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar, wakati Kundi la Mashauzi Classic, lilikuwa likiangusha burudani.
Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina moja la Addy ambaye anadaiwa kukubuhu kwa tabia hiyo chafu ya usagaji.
Ilisemekana kwamba mwanadada huyo alianza kumzengea Dida kwa kumsemesha huku akimuonesha pozi za kimahaba.

Dida akiwa mzigoni ndani ya ofisi za Times Fm.
Licha ya mtangazaji huyo kumpuuza, Addy alifika mbali na kuanza kumshtua kwa kutokea nyuma yake kwa kumtekenya huku akimkonyeza na kumshawishi waongee vizuri.
Kutokana na vitendo hivyo, Dida alipandwa na hasira na kuchukua chupa kutaka kumpasua ndipo Addy naye akawa anahangaika kujitetea na kusababisha vurugu katika eneo hilo, shukrani ziwaendee wasamaria wema waliwatuliza.
Akizungumza na Risasi Jumamosi mara baada ya kutulizwa, Dida alisema:
“Huyu dada ni muda mrefu alikuwa akinisumbua hapa ukumbini, mwanzo nilikuwa sijajua anachotaka kumbe ni mshenzi kabisa, anataka kunifanya vitendo vya kisagaji, amenikera sana.”




May 9, 2014

JAQUELINE WOLPER AONGELEA KUHUSU KUBADILI DINI, KUACHANA NA USAGAJI

Ni muda mrefu  kidogo  baada  mwigizaji Mtanzania Jaqueline Wolper kutosikika  akiyatoa ya moyoni kuhusu yote yaliyompata kwenye miezi iliyopita na kumfanya amiliki sana headlines za magazeti, blogs, website pia facebook na twitter huku wengi wakiwa na hamu ya kusikia akiyaongelea.
Kwenye Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa The Sporah show, Jack amekanusha kwamba yeye ni msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa kiume.
"Sasa hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za kiume, wengi walikua wanahisi lakini sijawahi kufanya vitendo vya usagaji na wala sijawahi kushawishiwa na mtu anaejihusisha na vitendo hivyo, boyfriend wangu hana tatizo na mavazi ya kiume ninayovaa… hatujawahi kupangiana mavazi"  Alisema  Wolper  na  kuongeza:
"Sijaolewa na wala sijawahi kuolewa, nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na usimuhukumu mtu bila kumuuliza"
Sporah: Ni kweli kwamba ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu unataka akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka ubadilishe dini ili upate hizo mali?


 J Wolper: Sio hivyo, dini nilikuja kubadilisha wakati nimeshapata mali, nilibadilisha mwishoni kabisa baada ya huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa, alinipa mali na vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana, unajua unaweza ukawa unachat na mtu mkapendana lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi, unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze kukushawishi mkapendana wakati yeye yuko mbali na wewe uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo wala sura bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri mpaka nikaona huyu ni sahihi nikabadilisha dini


Sporah: Ulifikiria kwamba dini yako sio nzuri au?
J Wolper: Kwa utamaduni wetu sisi Afrika, Tanzania ninavyojua hata kwa mama yangu imetokea, Mwanamke lazima ufate dini ya Mwanaume wako

Sporah: Lakini alikua bado hajakuoa?
J Wolper: Nilikua tayari nimeshajiona kama mke wake, ni mtu ambae alinipenda sana…

Sporah: Ulijichora na tatoo ya jina lake?
J Wolper: Kwa nini nichore jina la mtu kwenye mwili wangu, kwanza yeye ni Muislamu hapendi tatoo… nilibadili dini kwa mapenzi yangu mwenyewe kutokana na mtu niliekua nae na hawajui alivyonishawishi mpaka mimi nikabadili, sio kwa kulazimishwa….

Ninachojua mimi heshima ni kufuata dini ya Mwanaume ukishachumbiwa, haikua kama girlfriend na boyfriend… alikua ananifanya kama mke wake japo hatukua tumekutana


Sporah: Ulijisikiaje pale vitu havikwenda vizuri?
J Wolper: Mi naona ni sawa tu kwa sababu Mungu pia anapanga ila sikuumia sana, ningeumia kama mimi ndio ningekua nimetaka kuolewa ila yeye ndio alitaka ndoa, mimi bado mdogo… watu wa mitandao kwao ni big deal ila kwangu sio kitu

Haukuwa uamuzi mgumu, napenda sana kufata moyo wangu… siwezi kufata moyo wa mtu, wengi waliniambia sijui ukibadili dini tena sijui mashabiki wako sijui nini nini… NOOOO! sio kuhusu mashabiki, mimi ni mimi kama mimi sikupenda kilichotokea na bado niko chini ya wazazi wangu, vp ikitokea nimekufa nitazikwaje sijaolewa??! mi siwezi kumchezea Mungu ndio maana ukiangalia instagram yangu mimi kila Jumapili lazima niende kanisani

J Wolper: Nilikaa miezi miwili bila kwenda Msikitini wala Kanisani, nilikonda kwa sababu siwezi kukaa bila kusali na wazazi wangu nakua nawakosea, kuna neno mama yangu mdogo aliniambia baada ya kukaa na mama na kuongea nikasema ngoja nirudi kanisani, siwezi kufaidisha watu na kuacha wazazi wangu wakasononeka… nilibadili dini kwa heshima ya mchumba wangu lakini sasa hivi nimerudi kwa heshima ya wazazi wangu

J Wolper: Bado Dallas ni rafiki yangu mkubwa sana kwangu na ni mtu poa, haongei mapenzi maskini… ni rafiki yangu ni kaka yangu, hatuwezi tena kuwa wapenzi… nampenda bado.


SUPER STAR RAY C ALIVYOCHUNGULIA KIFO AFUNGUKA LIVE LIKE NEVER BEFORE!!

MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.


Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.


“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue, walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’ unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya kutosha.

“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia Ray C.


LULU "TURUHUSIWE KUIGIZA NUSU UTUPU ILI TUONYESHE UWEZO”

DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini ziwaruhusu wasanii waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.



Akitetea hoja yake mbele ya paparazi wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu utupu.

“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.





MSANII ANAELIPWA BEI KUBWA KULIKO WASANII WOTE WAKIKE HAPA BONGO HUYU HAPA

KWA mujibu wa baadhi ya mawakala wa filamu hapa Tz ni kwamba mwanadada huyu kwa sasa hakamatiki hapa bongo hususani katika filamu za Vichekesho, Baada ya kufululiza kutoa filamu kadha wa kadha zilizofanya kufuru sokoni sasa hivi apanda bei na kujikuta amekuwa wa gharama kuliko wasanii wote wa kike Bongo Movie's hasa unapotaka kumshirikisha katika filamu yako lazima jasho likutoke.


 Mlimbwende huyo ametokea kuvuma sana kwa kipindi kifupi na kuwa na mashabiki lukuki pia hayuko nyuma katika suala la kujitangaza mitandaoni.


Katika ukurasa wake wa instagram akipost chochote huonekana kupata maoni mengi mazuri kutoka wa mashabiki wake, Kitu ambacho kinampa moyo sana katika kazi zake na kujitambua kwamba yeye ni nani na anatakiwa afanye nini?.. Akiongea na mwandishi wa Masai Nyotambofu alifunguka hivi: Mimi hupenda kufanya uchunguzi kwanza kupitia mitandao kwamba nikifanya kipi watu wangu watakifurahia? Nafikiri ndio chanzo kufanya vizuri, Alisema nisha.

MREMBO JOKATE AANIKA SIFA ZA MUME MTARAJIWA....JE UNAZO? CHEKI HAPA


Mtoto mzuri kunako anga la watangazaji bongo, jokate mwegelo ameibuka na kuanika sifa za mwanaume ambaye anafaa kuwa mume wake.



Mtoto mzuri kunako anga la watangazaji Bongo, Jokate Mwegelo.
Akipia stori na paparazi wetu juzi jijini Dar, Jokate alisema anapenda mwanaume ambaye atajua kutafuta fedha kwa nguvu zote, awe anajua kubembeleza na awe na nidhamu kwa wazazi wake.


“Sifa ya mume ninayemtaka, anapaswa kuwa mtafutaji wa fedha, sipendi mwanaume asiyependa kutafuta, awe anajituma kwa kazi zake na kwa mpenzi au familia yake na pia ajue kunibembeleza,’’ alisema Jokate.