Ndugu zangu
naamini wote ni wazima wa afya njema.
Suala
ninalozungumzia leo litawahusu sana wasanii wa tasnia hii ya picha jengefu.
Kama nilivyoeleza siku zilizopita kuwa sana hii ni kazi kama zilizo kazi
nyngine kala kazi ina miiko na sheria zake za kazi.
Kama ilivyokuwa
katika kazi zingine kuwa huwezi ukaenda hazini kwa muda wako unaotaka wewe au
huwezi kwenda kazini ukiwahi umelewa au
ukwenda kazini alafu ukiagiza pombe na kuanza kunywa muda kazi lakini tabia hii inajitokeza kwa baadhi
yawasanii wetu wa hapa nyumbani Tanzania.
Sasa sijui
wanafanya hivi kwa sabababu hawajijui
wao ni kina nani? Au wanafanya makusudi kwasababu hawajui kama hiyo ni kazi
kama kazi nyingine.
Kwanini wasitenge
muda wa kazi na muda wa kufanya hiyo mambo yao. Hivi karibuni nimeshuhudia
msanii mkubwa kwa umri na msanii mkubwa
kwenye tansia hii ya filamu
akifikia location uishia bar na kuagiza pombe na kuanza kunywa hii ndiyo
ikanifanya nichukue kalum na kuandika haya yote.
Napenda kwasababu
wasanii wote popote pale walipo nchini
kujiheshimu na kuheshimiwa hii ni kazi, ili tujenge heshima mbele ya jamii yetu
inayotuzunguaka.
DARASA LA SANAA SEHEMU YA PILI
Kazi ya sanaa ni kazi ya taaluma kama zilivyo kazi zingine lakini kutokana na mfumo wa elimu wa tanzania somo la films halijawekwa ktk mitaala ya kielimu hapa tanzania na bahati mbaya vyuo vinavyotoa elimu ya juu ya filamu ni south africa na ghana pekee
DARASA LA SANAA SEHEMU YA KWANZA
Ndugu zangu kwanza ningependa
kuwasalimu na nina amini kuwa wote ni wazima.
Napenda kwa leo nizungumzie swala dogo sana katika sanaa hasa hii yangu ya
filamu. Leo napenda kutaka kutafsiri neon
mwigizaji nimekuwa nikipita sehemu nyingi ndani ya nchi
hii ninaitwa muigizaji au huyu anaigiza.
Tafasiri ya neno ili muigizaji inanitia shaka kidogo mfano waingereza wenzetu wanatumia neon actor
au actress. neno actor ni kwa muigizaji mwanaume na neon actress ni kwa muigizaji mwanamke lakini hapa nyumbani wote tunaitwa waigizaji. Tafsiri ya neno actor au actress ukiileta katika
lugha yetu ya kiswahili unaweza kupata tafsiri zisizo rasmi nyingi
sana napenda kutoa mfano mmoja mdogo sana:
Mfano ukisimama mbele ya kioo nafikiri utakacho kiona ni taswira halisi ya
muonekano wako mwenyewe, utakacho kifanya chochote ndivyo hivyo hivyo ile taswari itakavyo fanya, je kioo nacho
kitakuwa kinaigiza? Au kioo kinafanya
kile ambacho wewe unakifanya
kwa wakati ule?
Hapa ndipo napata shida ya neno muigizaji!
huyu muigizaji anaigiza nini? au anafanya mambo ambayo yanatokea
katika jamii inayomzunguka?sasa kwanini
umwite mwigizaji?
Wakati mwingine napenda kukubaliana na waingereza kuita waingizaji actor /
actress.
Kwa leo nitaishia hapa tutakutana tena wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment