DARASA LA SANA
SEHEMU YA TATU!
Naamini ndugu zangu wote ni wazima wa afya tele.
Leo napenda kuzungumza suala la hisia linavyoweza kuvuruga
mahusiano ya mtu na mwenzi wake. Hisia
ni mawazo ya mtu nwenyewe, lakini
hisia inaweza ikawa kweli au si kweli unaweza kuhisi mpenzi wako anakusailiti
inje.
Hii inaweza ikawa kweli au si kweli najua unaweza ukawa
shuhuda wa kuona ua kusikia mke au mume au mke wa mtu kusikia mke au mme
kutembea na mtu mwingine nje ya ndao.
Mfano ulio hali “Rafiki yangu juma ni mfanyakazi wa
nyumba moja ya wageni hapa jijin dar, kila siku akirudi kutoka kazini anakuja na story mpya
akishuhudia wake na waume za watu wakipishana kwenye kolido ya nyumba hiyo wakiingia na kutoka.
Wakati mwingine
anashuhudia ugomvi wa fumanizi. Kutokana na hadithi hizi za Juma wakati mwingine nataka kuamini mpenzi wangu
ananisaliti nje lakini wakati mwingine napoteza hisia zangu.
Kwanini tumekuwa na hisia za
wapenzai wetu kutusaliti?
Siku moja rafiki yangu wa karibu sana alikuja kuniomba
ushauri kuwa anahisi mpenzi wake siku hizi amebadilika , wakati mwingine akimuomba haki yake ya ndoa mpenzi wake
hujibu nimechoka.
Siku za nyuma mpezi wake alikuwa akimpagia simu akiwa kazini
mara msili hadi tatu kwa siku hata kama jambo analompigia ni la kipumbavu
lakini siku hizi anaweza kutopiga kabisa.
Anaendelea kwa kusema kuwa siku hizi ata akichelewa kurudi
nyumbani mpenzi wake hamuulizi chochote
ule wivu wa mwanzo umepungua kabisa.
Zamani walipokuwa wamekaa pamoja simu yake ya mkononi ikiita
alitaka kujua ni nani aliyempigia lakini cha kushangaza mpezi wake huyo anaweza
ata kuondoka asisikie kinachoongeewa.
Kwa maana hiyo anapata hisia kuwa mpenzi wake huyo
anamsaliti. Alitaka ushahuri afanyeje? Nikamjibu ngoja suala ili nilipeleke kwa
wadau ili wachangie.
Ndugu zangu naomba tumshaui huyu ndugu yetu afanyaje?
Suala la wanaume wa kisasa kukwepa majukumu linashika kasi. Mwanamke anapomfuata mwanaume na kumwambia kuwa ana ujauzito wake majibu yake huwa makali na mapenzi huishia hapo iweje ukatae mimba wakati mlikuwa hamtumii kinga
DARASA LA MAPENZI SEHEMU YA KWANZA.
Simu huwaachanisha wapenzi.
Kwanza ningependa kuwasalimu ndugu zangu na wadau wa safu hii ya darasa la mapenzi.
Wakati mawasiliano ya
simu ni njia rahisi ya kurahisisha shughuli zetu za kila siku lakini simu
imekuwa ni moja ya vitu vinavyosababisha mahusiano ya watu kuvunjika.
Wataalamu wa mapenzi wanakwambia wivu ni ishara ya mapenzi
lakini wivu ukizidi sana nayo ni kero.
kumekuwa na tabia ya baadhi ya
wapenzi wanapokuwa wamekaa na wapenzi wao wengine uweka simu zao silence,
wengine huamua kuzima kabisa ili kuepuka kugombana na wapenzi wao.
Njia hii kwangu siwezi kuiunga mkono hata kidogo kwani kama
tabia yako siyo nzuri siyo nzuri tu cha msingi hapa ni kuwekana wazi wote
wawili na kila mmoja amwamini mwenzi wake
ingawaje najua siyo rahisi sana kuliami ili.
Simu hivi sasa zimekuwa zina mambo mengi sana kama zile
whats-up, facebook, twitter,ukiwa umekaa na mpenzi wako mahali ukanza kuchati
na mtu kwa kutumia simu huo utakuwa ni mwanzo wa ugomvi tu, kwa maana kila
baada ya sekunde ujumbe mfupi unaingia ( sms) mpenzi wako hapo anaanza kuingiwa
na mashaka na baadae atataka kujua unachati na nani.
Inawezekana ukwa
unachati mambo ya kawaida tu lakini kwasababu ya wivu mtaanza kugombana tena
mbele za watu.
Ushauri wangu ukiona
mpezi wako hapendi mambo ya kuchati bora
upige simu uongee na mtu wako au utafute
muda mwingine wa kuchati, lakini kama
wote mna aminiana hakuna mtu wa kumtilia mwenzake shaka.
Najua mapenzi ni kama mfano wa kidonda ambacho ukitumia dawa ya maumivu kinapoa lakini kupona hakiponi.
Basi ndugu zangu kwa
leo niishie hapa tutaendelea wiki ijayo
na mada hii hii ya simu kwani ni ndefu sana.
No comments:
Post a Comment