MUNGU
mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’,
amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na
tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Staa wa muziki wa
Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya
Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka
mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala,
Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha
yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama
ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema
kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa
kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na
kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.
Staa
huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa
tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi
kuamini baada ya madaktari kunipima na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue,
walinishangaa sana hata namna nilipofika pale na kwamba sikutumia dawa yoyote
ya kutuliza maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni lazima utatafuta tu dawa ya
kukufanya upoze maumivu.
“Madaktari
wengine wakatishika zaidi maana walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’
unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika
magonjwa ya ajabu na yanayostahili kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni
ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa iwe macho sana maana haufai hata
kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia utapoteza maisha ya
Watanzania kibao kama hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania elimu ya
kutosha.
“Mateso
niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na
kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa
nchi basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada za haraka kuhakikisha wanapata
chanjo kwa ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa mchana na dawa yake ni panadol
tu!” alimalizia Ray C.
No comments:
Post a Comment