Aunt Ezekiel.
BAADA ya wiki iliyopita kumaliza mahojiano na Miss Tanzania 2006
aliye pia mwigizaji wa sinema za Bongo, Wema Isaac Sepetu, wiki hii tunaye
supastaa mwingine.
Anaitwa Aunt Ezekiel Grayson, si jina geni kwa
wadau mbalimbali wa burudani nchini. Ni mrembo ambaye amepata jina kubwa
kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka saba iliyopita.
Msanii
huyo ambaye ni mtoto wa damu wa aliyekuwa mchezaji mahiri wa Simba Sports Club
‘Wekundu wa Msimbazi’ marehemu Ezekiel Grayson.
Aunt
Ezekiel amepitia maisha magumu sana kabla
ya
kufika alipo leo. Ili kujua maisha yake halisi ungana na mimi, Imelda Mtema.
Mwandishi:
Mambo Aunt? Natumaini uko mzima. Mimi ningependa kujua zaidi historia ya maisha
yako kuanzia ulikotokea hadi ulipo sasa.
Aunt:
Duu! Sawasawa! Mimi nimezaliwa mwaka 1988 hapahapa jijini Dar es Salaam.
Ni mtoto wa pili kwa mama yangu mzazi kwa sababu kwa baba nina
ndugu zangu wengine.
Mwandishi:
Kwa hiyo una maanisha kabla ya baba yako kuwa na mama yako alikuwa na mwanamke mwingine?
Aunt:
Ndiyo.
Mwandishi:
Wakati huo ulikuwa ukiishi hapa Dar es Salaam sehemu gani?
Aunt:
Nilikuwa nikiishi Ilala na nilipata elimu yangu ya msingi katika Shule ya
Msingi Bunge mwaka 1995 mpaka 1998, nikaenda kumalizia Kisarawe, Pwani.
Mwandishi:
Kwa nini ulikwenda kumalizia huko? Ilikuwa bording (shule ya bweni)?
Aunt:
Hapana, baba yangu alipata matatizo akapelekwa jela hivyo kukawa hakuna mtu wa
kunilipia ada pale Shule ya Bunge, hivyo wakanipeleka kule kwa babu na bibi
yangu.
Mwandishi:
Mama yako alikuwa wapi kipindi hicho?
Aunt:
Mama yangu alifariki dunia mwaka 1995, hivyo nilibaki na baba na ndugu zangu
wengine.
Mwandishi:
Sasa hukuona kama kuna tofauti wakati ulikuwa umeshazoea maisha ya mjini?
Aunt:
Tofauti ilikuwepo kubwa sana lakini ilibidi nizoee niweze kusoma tu maana
sikuwa na jinsi.
Mwandishi:
Ilikuwaje baada ya kumaliza shule, uliendelea kuishi Kisarawe?
Aunt:
Yaani maisha yalizidi kuwa magumu sana, niliendelea kukaa huko lakini baadaye
ilibidi nitoroke.
Mwandishi:
Kwa nini ulitoroka, ulikuwa ukiteswa?
Aunt:
Hapana, nilipomaliza tu shule kuna mwanaume alikuja kwa babu akasema anataka
kunioa.
“Sikuwa
tayari kabisa lakini kwa vile alikuwa na pesa ndugu zangu waliona bora niolewe
naye kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kunisomesha tena.
“Ilibidi
nitoroke, nikaja Gongo la Mboto (Dar es Salaam). Kuna sehemu inaitwa Mazizini.
“Nilisema
nije nitafute kazi yoyote ile, popote pale ili niweze kujinusuru na kuolewa
nikiwa katika umri mdogo.
Aunt
Ezekiel ametoroka nyumbani Kisarawe na kukimbilia Dar kutafuta kazi.
No comments:
Post a Comment