Ni muda
mrefu kidogo baada
mwigizaji Mtanzania Jaqueline Wolper kutosikika akiyatoa ya moyoni kuhusu yote yaliyompata
kwenye miezi iliyopita na kumfanya amiliki sana headlines za magazeti, blogs,
website pia facebook na twitter huku wengi wakiwa na hamu ya kusikia
akiyaongelea.
Kwenye
Exclusive interview na mtangazaji Sporah wa The Sporah show, Jack amekanusha
kwamba yeye ni msagaji japo mara kadhaa ameonekana akivaa kiume.
"Sasa
hivi nimepunguza sana kuvaa nguo za kiume, wengi walikua wanahisi lakini
sijawahi kufanya vitendo vya usagaji na wala sijawahi kushawishiwa na mtu
anaejihusisha na vitendo hivyo, boyfriend wangu hana tatizo na mavazi ya kiume
ninayovaa… hatujawahi kupangiana mavazi"
Alisema Wolper na
kuongeza:
"Sijaolewa
na wala sijawahi kuolewa, nilishawahi kubadili dini kweli… ni vitu vinatokea na
usimuhukumu mtu bila kumuuliza"
Sporah: Ni
kweli kwamba ulikutana na mtu ana uwezo wa kifedha na kulikua kuna vitu unataka
akununulie akasema hawezi kukufanyia mpaka ubadilishe dini ili upate hizo mali?
J Wolper: Sio hivyo, dini nilikuja kubadilisha wakati nimeshapata mali,
nilibadilisha mwishoni kabisa baada ya huyu mwanaume kuja kwetu akitaka kunioa,
alinipa mali na vitu vya thamani kabla ya sisi kukutana, unajua unaweza ukawa
unachat na mtu mkapendana lakini hamjawahi kukutana… ni mzuri wa kukushawishi,
unajua sio rahisi mtu akiwa mbali aweze kukushawishi mkapendana wakati yeye
yuko mbali na wewe uko mbali, namsifia kwa uzuri wake… sio wa umbo wala sura
bali ana roho nzuri na alinitreat vizuri mpaka nikaona huyu ni sahihi
nikabadilisha dini
Sporah: Ulifikiria
kwamba dini yako sio nzuri au?
J Wolper: Kwa utamaduni
wetu sisi Afrika, Tanzania ninavyojua hata kwa mama yangu imetokea, Mwanamke
lazima ufate dini ya Mwanaume wako
Sporah: Lakini alikua
bado hajakuoa?
J Wolper: Nilikua tayari
nimeshajiona kama mke wake, ni mtu ambae alinipenda sana…
Sporah: Ulijichora na
tatoo ya jina lake?
J Wolper: Kwa nini
nichore jina la mtu kwenye mwili wangu, kwanza yeye ni Muislamu hapendi tatoo…
nilibadili dini kwa mapenzi yangu mwenyewe kutokana na mtu niliekua nae na
hawajui alivyonishawishi mpaka mimi nikabadili, sio kwa kulazimishwa….
Ninachojua mimi heshima
ni kufuata dini ya Mwanaume ukishachumbiwa, haikua kama girlfriend na
boyfriend… alikua ananifanya kama mke wake japo hatukua tumekutana
Sporah:
Ulijisikiaje pale vitu havikwenda vizuri?
J Wolper: Mi
naona ni sawa tu kwa sababu Mungu pia anapanga ila sikuumia sana, ningeumia
kama mimi ndio ningekua nimetaka kuolewa ila yeye ndio alitaka ndoa, mimi bado
mdogo… watu wa mitandao kwao ni big deal ila kwangu sio kitu
Haukuwa
uamuzi mgumu, napenda sana kufata moyo wangu… siwezi kufata moyo wa mtu, wengi
waliniambia sijui ukibadili dini tena sijui mashabiki wako sijui nini nini…
NOOOO! sio kuhusu mashabiki, mimi ni mimi kama mimi sikupenda kilichotokea na
bado niko chini ya wazazi wangu, vp ikitokea nimekufa nitazikwaje sijaolewa??!
mi siwezi kumchezea Mungu ndio maana ukiangalia instagram yangu mimi kila
Jumapili lazima niende kanisani
J Wolper:
Nilikaa miezi miwili bila kwenda Msikitini wala Kanisani, nilikonda kwa sababu
siwezi kukaa bila kusali na wazazi wangu nakua nawakosea, kuna neno mama yangu
mdogo aliniambia baada ya kukaa na mama na kuongea nikasema ngoja nirudi
kanisani, siwezi kufaidisha watu na kuacha wazazi wangu wakasononeka…
nilibadili dini kwa heshima ya mchumba wangu lakini sasa hivi nimerudi kwa
heshima ya wazazi wangu
J Wolper:
Bado Dallas ni rafiki yangu mkubwa sana kwangu na ni mtu poa, haongei mapenzi
maskini… ni rafiki yangu ni kaka yangu, hatuwezi tena kuwa wapenzi… nampenda
bado.