Mkutano wa kurasimisha
sekta ya filamu na muziki uliofanyika Jana katika ukumbi wa vijana kinondoni
jijini Dar umeondoka na Azimio moja kuu tarehe 23 January 2014 wasanii wa
filamu na muziki watafanya maandamano kuanzia vijana mpaka wizara ya habari
utamaduni na michezo kwenda kukabidhi Sera ya filamu na muziki ili iperekwe
bungeni kutungwa sheria.mkutano huo uliandaliwa na TRA. COSOTA. BASATA.TAFF na
Shirikisho la Muziki.
www.shijamovies.blogspot.com
December 31, 2013
WASTARA AMLIZA MAMA SAJUKI
Mwigizaji wa bongo movie
na Mke wa marehemu Sajuki amemfanya Mama Mzazi wa marehemu Sajuki kutokwa na
machozi baada ya kumuona Wastara. Wastara yupo songea mkoani ruvuma kwa ajili
ya dua maalumu ya kumuombea marehemu Mume wake Sajuki itakayofanyika Alhamisi wiki hii.
December 27, 2013
BONGO MOVIE KUFANYA MAANDAMANO
Wakati wasanii wa
filamu wakiwa wamepanga kufanya maandamano ya kupinga wizi wa kazi za wasanii
kesho jumamosi katibu mkuu wizara ya habari utamaduni na michezo amewaomba
wasanii hao kusitisha maandamano na kuwaita wizarani kwa majadiliano na
kuangalia namna ya kulitatua tatizo hilo.
Akizungumza katika blog
hii msanii wa filamu hapa nchini Issa Musa " cloud" amethibitisha
kupokea barua hiyo ya mwaliko siku ya jumatatu 30/12/2013
WASTARA AMKUMBUKA SAJUKI
Zikiwa zimebaki Siku 6
kutimiza mwaka mmoja tangu marehemu sajuki atangulie mbele za haki.
Msanii wa filamu na
aliyekuwa mke wa sajuki Wastara yuko njiani kuelekea songea kijijini kwa
marehemu sajuki kwa maandalizi ya dua ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu sajuki
alipofariki.
Marehemu sajuki
alifariki tare he 2/1/2013 katika hospitali ya muhimbili baada ya kuugua kwa
muda mrefu.Wastara anaomba mashabiki wake wamuunge mkono katika dua hiyo
December 23, 2013
ZAWADI YA X-MASS KUTOKA KWA MALIKIZOH
Msanii wa
kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizoh ameachia ngoma yake mpya
ijulikanayo kama SUPER HERO.
“Napenda kuwaomba mashabiki wangu wa muziki kuendelea
kuniunga mkono katika kazi zangu nyingine zijazo”alisema malikizoh.
FUNGUA
HAPA UONE HIYO KITU KALI>>>>
https://www.youtube.com/watch?v=hO0d3pGmCVY&feature=youtube_gdata_player
JACKLINE WOLPER ARUDIA DINI YAKE
Mwaka uliopita
ilisemekana kuwa mwana dada huyo alibadilisha dini kutoka na mpenzi wake wa
zamani Bwana Abdala Mtoro"Dallas" kuwa ni Muislamu.
Kwa sasa mwana dada huyo
kila jumapili anashika biblia na kuingia kanisani.
December 21, 2013
HEMED NA MLELA HAWANA UGOMVI
Kutokana na tetezi
zilizozagaa mjini hapa kuwa waigiza wa filamu za kibongo Hemed Suliman”PHD” na Yusuf
Mlela kuwa wana bifu la kufa mtu si za kweli kuthibitisha hilo wasanii hao.
Walikutana katika ofisi
za Steps Entertaiment kampuni inayosambaza filamu za kibongo na kupeana mikono
kwa furaha tele.
BONGO MOVIE KUFANYA MAANDAMANO
Wakati wasanii wa filamu
nchini wakifikiria kurudi kwenye michezo ya tamthilia wameamua kufanya maandamano
katika mkoa wa dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 28 mwezi huu.
Akizungumza kwa niaba ya
wasanii wenzake Issa Musa maarufu kama “cloud” amesema lengo la maandamano hayo
ni kupiga kelele juu ya wizi wa kazi za wasanii ili serikali isikie kilio chao
na kutoa sheria kali kwa wale wote watakaobainika kuiba kazi zao wakati huo huo
jeshi la polisi kanda ya DSM tayari imeisha toa kibali cha maandano hayo.
December 19, 2013
JELA IMENIFUNZA MENGI.
Mwigizaji Mrembo wa Bongo
Movie Elizabeth Michael “lulu” amesema kitendo cha kukaa mahabusu takribani
miezi kumi amejifunza mambo mengi sana.
Lulu ambaye alikuwa mahabusu ya segerea baada
ya kifo cha marehemu Steven Kanumba kwa sasa lulu anatamba na filamu yake ya Foolish
Age.
December 18, 2013
WASANII KURUDI KWENYE TAMTHILIA
Baada ya
wizi wa kazi za wasanii kupamba moto nchini,makampuni ya usambazaji wa Filamu kutishia kufunga makampuni yao.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wanataka kurudisha michezo ya TV Kama zamani.kipindi cha nyuma kulikuwa na makundi kama Kaole ,Mambo hayo, Fukuto yaliyofanya vizuri sana kwenye luninga. Msanii maarufu nchini DR Cheni alisema ni bora wasanii tukarudia michezo ya TV kuliko filamu ambazo zinaibiwa na kupata hasara.
Katika kufanya
kwa vitendo msanii mnene hapa nchini JB amesema yeye anaingia kambini
kutengeneza tamthilia.
December 17, 2013
TUNDA MAN AJA NA ZAWADI YA MWAKA MPYA
Msanii wa
bongo fleva Khalid Ramadhani ametoa nyimbo yake mpya inayojulikana kama
msambingungwa.
Tunda amesema jina la msambingungwa ni jina la msichana aliyekuwa anamsumbua kwa muda mrefu
WEMA MAHAKAMANI TENA
Baada ya
Mahakama ya Mwanzo kawe kumuachia kwa faini ya laki moja mwana Dada Wema Sepetu
mlalamikaji katika kesi hiyo bwana Gudluck Kayumbu ameibuka na kusema
hakuridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo na anakusudia kukata
rufaa.
Wapenzi wa Mwana Dada Wema Isaack Sepetu wameibuka na kusema Meneja huyo anatafuta kick kupitia jina la Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu
December 16, 2013
Matukio ya mwaka 2013 => Bongo movie wampoteza sajuki
2 /01/ 2013 tulimpoteza msanii nguli wa Filamu
nchini Juma Kilowoko Sajuki.
Bado siku chache kutimiza Mwaka mmoja tangu tasnia
ya Filamu kuondokewe na msanii maarufu Sajuki.
DEAGRATIUS SHIJA ateuliwa kuwa meneja wa MALIKIZO
Msanii wa kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizo amemteuwa Muigizaji wa
bongo movie Deogratius Shija kuwa msimamizi wa kazi zake za muziki.
Deogratius Shija ndio meneja wa Malikizo
December 13, 2013
MIKE SANGU APATA USUMBUFU.
Aliyekuwa Mume wa
muigizaji wa Bongo Movie Ndumbangwe Misayo “Thea” Mike Sangu amefunguka na
kusema kuwa tangu waachane na mkewe Thea amekuwa akisumbuliwa na
kupigiwa simu na wanawake wanaomtaka kimapenzi.
“Tangu watu walipojua
tumeachana na Thea siku za hivi karibuni nimekuwa nikisumbuliwa sana na wanawake
wengi”
Alipoulizwa kama
anampango wowote wa kurudiana na Thea Mike alijibu "namuachia mungu tu kwani
sikuona sababu yoyote ya Thea kuondoka nyumbani kwangu. kwakweli napata shida sana
nimekuwa mtu wa kula hotelini na sina muda mzuri wa kula nyumbani kwangu ili
linanipa shida sana " ndoa ya Mike na Thea
ni ndoa iliyodumu miaka mitatu tu alisema Mike
December 12, 2013
MALIKIZO KUTOA SUPER HERO
Msanii wa
kitanzania anaeishi nchini Australia Malikizo anatarajia kuachia ngoma yake
mpya itakayojulikana kwa jina la SUPER HERO.Malikizo anaendelea kusema ngoma
yake hiyo ni moja kati ya ngoma kali aliyoifanyia katika jiji la Perth nchini
humo.
Malikizo anaendelea kufunguka na kusema kuwa SUPER
HERO NI ZAWADI ya X-MASS kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva. ”Ngoma ya SUPER
HERO itakuwa hewani katika vituo mbalimbali vya Redio na TV. Malikizo yupo
nchini Australia kwa masomo ya Muziki na Filamu.
“Napenda kuwaomba mashabiki wa muziki kuipokea ngoma yangu hii mpya’ Alisema Malikizo.
BURIANI MZEE HILUKA.
Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na rais wao wa TAFF Bwana Saimon Mwakifamba jana ni miongoni
mwa watu waliojitokeza kumzika Baba mzazi wa katibu wa shirikisho la Filamu
Tanzania “TAFF” bwana Bishop Hiluka uko boko jijini Dar es salaam.
Mzee Hiluka alifariki katika Hospitali ya Hindu Mandal kwa ugonjwa wa
moyo.
“Kwakweli
nimefarijika sana kuwaona wasanii wenzangu wamekuja kumzika Baba yangu” alisema
Bishop huku akitoa machozi kwa uchungu
December 11, 2013
TAARIFA ZILIZO ENEA KUWA MZEE SMALL KAFA SI ZA KWELI NI UONGO..HII NDO KAULI YA MTOTO WAKE MUDA HUU
KUNA TAARIFA ZIMEENEA USIKU HUU KUWA MZEE SMALL KAFARIKI,HIZO TAARIFA SI ZA KWELI BALI NI UONGO MTUPU ULIO SAMBAZWA MITANDAONI..MTANDAO HUU
WA THECHOICE ULIWEZA KUONGEA NA MTOTO WAKE USIKU HUU AITWAE MAHAMOUD NA KUTHIBITISHA KUWA BABA YAKE YU HAI HAJAFARIKI. "BABA YU MZIMA NA WALA HAJAFARIKI KWANI NIMETOKA KUMJULIA KHALI MDA SI MREFU NA NI MZIMA ANAENDELEA VIZURI NA HIZO TAARIFA NI ZA UONGO "
http://www.thechoicetz.com/2013/12/breaking-newzzztaarifa-zilizo-enea-kuwa.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29&m=1
WA THECHOICE ULIWEZA KUONGEA NA MTOTO WAKE USIKU HUU AITWAE MAHAMOUD NA KUTHIBITISHA KUWA BABA YAKE YU HAI HAJAFARIKI. "BABA YU MZIMA NA WALA HAJAFARIKI KWANI NIMETOKA KUMJULIA KHALI MDA SI MREFU NA NI MZIMA ANAENDELEA VIZURI NA HIZO TAARIFA NI ZA UONGO "
http://www.thechoicetz.com/2013/12/breaking-newzzztaarifa-zilizo-enea-kuwa.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+blogspot%2FGDSbw+%28TheCHOICE%29&m=1
December 9, 2013
KATIBU WA TAFF APATA PIGO
Katibu wa shirikisho la filam Tanzania “TAFF”Bwana Bishop Hiluka
amepata pigo baada ya kufiwa na baba
yake mzazi Mzee Hiluka.
WASTARA AFUNGUKA
Wakati wadau wa tasnia ya filamu nchini wakimshauri msanii wa
filamu Deogratius Shija kumuoa msanii mwenzie Wastara Juma.
Kuna tetesi kuwa
mwana dada huyo mjane amekuwa na
mahusiano ya kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha ACTION and CUT bwana Bond bin sinnan. Wastara amesema
kuwa muda siyo mrefu mrefu atamtambulisha mpenzi wake mpya.
December 6, 2013
WIZI WA KAZI ZA WASANII.
kutokana na
wimbi kubwa la kazi za wasanii hususani filamu imesababisha baadhi ya makampun
ya wasambazaji kufunga virago.akizungumza kwa
niaba ya wenzao mtayarishaji na msanii wa filamu za kibingo Vicent Kigosi “RAY”
amesema hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la wizi wa kazi za filamu.
Ray ameendelea
kusema kuwa kama hali hii itaendelea hivi wasambazaji wote watayafung makampuni
zao na hakutakuwa na filamu hata moja sokoni.Ray anaomba wadau pamoja na
serikali kupiga marufuku kwawizi wa kazi za wasanii kame wanavyopiga vita
uuzaji wa madawa ya kulevya
MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.
Katika kukabiliana na janga la ukimwi nchini taasisi ya MKAPA FOUNDATION imewataka wasanii wa filamu na wanamuziki wa kizazi kipya kushikamana kwa pamoja na kuelimisha jamii katika suala zima la maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Akiendelea kufafanua zaidi MH WAZIRI amesema wasanii wana nguvu ya ushawishi mkubwa katika jamii ya leo.
MKAPA FOUNDATION iliandaa majadiliano hayo katika siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika katika hoteli ya protea ya jijini Dar es salaam.
R.I.P NELSON MANDELA 1918/2013
Wasanii wa bongo fleva na bongo movie
wanatoa pole kwa familia na serikali ya Africa kusini kwa kuondokewa na mzee wao Nelson
Mandela.
Subscribe to:
Posts (Atom)